Burkina Fa­­so Mshindi wa Tatu Afcon 2017..!!!


Timu ya Taifa ya Burkina Faso imekuwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Gabon, baada ya kuifunga Ghana 1-0 katika Uwanja wa Port-Gentil.

Mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Alain Traore katika dakika ya 89 uliomshinda kipa wa Black Stars, Richard Ofori ulitinga kimiani na kuifanya Burkina Faso kutwaa nafasi hiyo, ambayo Ghana imekuwa ikiitawala kwa muda mrefu.

Ghana ilitolewa na Cameroon katika hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kipigo cha 2-0, huku Burkina Faso ikiondoshwa na Mafarao wa Misri kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Leo usiku macho na masikio yataelekezwa Gabon kushuhudia fainali ya kukata na shoka baina ya miamba ya Cameroon na Misri, mechi ambayo itaamua bingwa wa mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika.

Misri ni mabingwa wa kihistoria wa Afcon kwa kuwa wametwaa taji hilo mara saba, huku Cameroon maarufu kama Indomitable Lions wakitwaa ubingwa huo mara nne.

Read More »

Waliopasua Kidato cha Nne Gharama Yake Haikamatiki

“Usione vyaelea vimeundwa.” Huo ni msemo wa wahenga unaomaanisha kila mafanikio yana maandalizi yasiyo ya kubahatisha.

Msemo huo unaendana na kilichotokea katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa wiki hii, ambayo katika shule 10 zilizofanya vizuri hakuna hata moja yenye maandalizi ya lele mama. Shule nyingi kati ya hizo ada zake ni kuanzia Sh8 milioni hadi 10 kwa mwaka.

Uchunguzi  umebaini kuwa shule hizo zote ni zenye majengo mazuri, walimu wazuri na wenye motisha, maabara zilizokamilika, sehemu nzuri za kulala na zinazotoza ada zaidi ya Sh2.5 milioni, mbali ya gharama nyingine za chakula, malazi na vitabu.

Shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizoshika nafasi za kwanza ni Feza Boys (Dar es Salaam), St. Francis Girls (Mbeya), Kaizirege (Kagera), Marian Girls (Pwani), Marian Boys (Pwani), St Aloysius  Girls (Pwani), Shamsiye Boys (Dar es Salaam), Anwarite Girls (Moshi), Kifungilo Girls (Lushoto) na Thomas More Mashrina (Dar es Salaam).

Wanafunzi wa Sekondari Kaizirege Junior iliyoshika nafasi ya tatu, kila mmoja analipa Sh2.5 milioni za ada. Malipo hayo kwa baadhi ya shule hayahusishi gharama za malazi, chakula na vitabu.

 Shule ya Wasichana ya St. Francis ili mwanafunzi ajiunge nayo, anatakiwa kulipa Sh2.2 milioni za ada kwa mwaka, huku akitakiwa kulipa katika mikupuo minne mbali na mahitaji mengine.

Mwanafunzi wa Feza Boys ada ni Sh2.9 milioni, lakini ikijumlishwa na gharama za chakula, malazi na vifaa vya masomo, inafika zaidi ya Sh8 milioni.

Kuhusu Thomas More Machrine ada ni Sh3.6 milioni kwa kidato cha nne na cha sita. Hivyo, mwanafunzi akisoma kwa miaka minne anatakiwa kulipa Sh14.4 milioni.

Uchunguzi huo ulibaini mwanafunzi anayesoma shule za Marian Boys na Girls kidato cha kwanza hadi cha nne, anatakiwa kulipa Sh2.8 milioni.

Kwa wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo kwa ajili ya kidato cha tano na sita, watalipa Sh2.7 milioni hiyo ina maana watatakiwa kulipa Sh5.4 milioni kwa miaka miwili.

Shule ya Anwarite ya Kilimanjaro ada yake ni Sh1.9 milioni,  hivyo kwa miaka minne mwanafunzi analazimika kulipa Sh7.6 milioni.

Mmoja na viongozi wa shule hizo ambaye hakuwa tayari kutajwa, alisema shule hizo zinatoa elimu bora na mazingira mazuri ya kuishi kwa mwanafunzi, hivyo badala ya kuonekana kero zingepewa ruzuku.

Read More »

Mama ‘Aliyemwaga Mboga’ Mbele ya Rais JPM Atiliwa Shaka..!!!Soma hapa

TAHARUKI iliyojitokeza juzi mbele ya Rais John Magufuli, kwa mkazi wa Tanga, Swabaha Shosi kudai kudhulumiwa mirathi ya mumewe, imeibua sintofahamu mpya baada ya waliojiita familia ya huyo mume, kujitokeza na kutangaza kutomtambua Swabaha.

Akizungumza jana Tanga na mwandishi , mwanafamilia aliyejitambulisha kuwa mtoto katika familia hiyo, Saburia Mohamed (37), alidai mara ya kwanza kumwona Swabaha, ilikuwa siku ya kumaliza msiba wa baba yake.

Juzi katika kilele cha Siku ya Sheria, Swabaha huku akilia mbele ya Rais Magufuli na uongozi wa juu wa Mahakama na Polisi, alidai kunyimwa haki ya mirathi ya mumewe na vyombo vya kutoa haki nchini.

Swabaha ambaye alifanikiwa kugonga vichwa vya habari juzi na jana, alitaja vyombo vilivyomnyima haki kuwa ni Polisi, Mahakama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Lakini jana Saburia, aliyejitambulisha kwa mwandishi wa gazeti hili kama mwanafamilia, alidai kutomtambua na kueleza kuwa siku ya kwanza kumwona, ilikuwa ya kumaliza msiba wa baba yao.

Saburia alidai kuwa siku hiyo Swabaha alitambulishwa kama binamu yao kwa shangazi yao aliyeko Mombasa na alikuwa akitoka eda Dar es Salaam baada ya kufiwa na mumewe.  

"Yule mama sisi kwa mara ya kwanza tulitambulishwa siku ya kumaliza msiba wa baba yetu tukiwa kwenye kikao cha familia, alifika saa sita mchana, tukaambiwa kuwa ni mjomba wa marehemu baba na ametoka eda Dar es Salaam ya aliyekuwa mumewe naye alithibitisha hilo," alidai.

Hata hivyo, Saburia alidai kuwa wakili wa familia alipokuwa akisoma wosia wa marehemu, Swabaha alimnyang'anya wosia huo na kukimbia nao baada ya kuona jina lake halimo.

Mtoto huyo alidai kuwa mwaka 2012 ilifunguliwa kesi ambayo ilimalizika kwa kufutwa Desemba 15, mwaka juzi na mwaka huo huo familia ilipeleka maombi Mahakama ya Mwanzo, kumpendekeza Saburia awe msimamizi wa mirathi.

Alidai kabla ya kupewa usimamizi, Swabaha alijitokeza mahakamani na kupinga kwa madai kuwa anayependekezwa kusimamia mirathi hiyo si mtoto halali wa marehemu.

Saburia alidai kuwa mama huyo hakuwa sahihi kupeleka taarifa kwa Rais, kwani kesi yao bado inaendelea Mahakama Kuu, ambako inasikilizwa na Jaji Amour Said Khamis na bado hukumu haijatolewa.

Alidai kuwa yeye na familia yake hawana vitisho vyovyote kwa mama huyo na familia ilipatwa na butwaa aliposema anahitaji ulinzi kwa kuwa anatishwa.

Mtoto huyo alielezea masikitiko yake kuwa ameumia baada ya Swabaha kumtangaza mbele ya Rais kuwa anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya, kitu ambacho si kweli na kwamba yuko tayari kufanyiwa uchunguzi wa jambo hilo.

"Mimi ni mfanyabiashara wa nguo na nina duka langu la nguo barabara ya 14, ameniumiza sana pamoja na familia yangu kwa kusema nauza dawa za kulevya. Naomba Serikali iliangalie hili, kwani niko tayari kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma hizi," alidai.

Mbali na Saburia, mwandishi wa habari hii alizungumza na aliyetambulishwa kuwa mke mkubwa katika familia hiyo, Mariam Juma ambaye alidai kuwa hamfahamu Swabaha.

"Mimi ninamfahamu mama yake ambaye ni wifi yangu na anaishi Mombasa, yeye sijawahi kumwona. Sasa nilishangaa kubadilika na kusema kuwa ni mke wa marehemu na kudai ananyanyasika kwa kudhulumiwa mirathi," alisema Mariam.

Aliitaka Serikali iingilie kati suala hilo ili wapate haki zao yeye na familia yake, ambayo ina watoto tisa na wake wawili.

Juzi Rais Magufuli aliwaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashitaka, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Mahakama kupitia Jaji Kiongozi, kushughulikia jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuhamishia kesi hiyo Mahakama ya Juu ili uamuzi ufanyike.

Read More »

HUU HAPA WIMBO WA MWANA FA ULIOTIMIZA MIAKA 15 TANGU KUANZA KUCHEZWA REDIONI

Hit maker wa ‘Dume Suruali’, Mwana FA afunguka juu ya ngoma yake iliyotimiza miaka 15 tangu kuanza kuchezwa katika redio mbalimbali. Ni wazi kabisa Dume suruali ni wimbo wake unaofanya vyema ndani ya nchi na nje pia.
Mwana Fa ni moja kati ya marapa bora walioko chini ya kivuli cha hip hop, ambaye tangu aingie katika ramani ya muziki wa kizazi kipya hajawahi kupoteza ubora wake.
Mwana Fa amekuwa msanii tofauti zaidi na wengine katika upande wa kutunza rekodi za muziki wake. Ni wazi changamoto moja wapo ya wasanii wa kizazi kipya ni kutokujua kutunza rekodi ya mambo yote katika muziki wao.
Kupitia akaunti yake ya ‘Instagram’ Mwana Fa ameweka wazi rekodi zake katika maisha yake ya muziki, ambapo ameeleza
Mwana Fa
“2/2/2017 Ni miaka 15 ‘cash’ toka mara ya kwanza wimbo wangu umepigwa redioni..Ingekuwa Vipi feat Jay Mo produced by Bon Luv nashukuru! Lakini pia hakuacha kuweka wazi wake ambao anaupenda zaidi ambao ni ‘Mfalme’ akiwa amemshirikisha G Nako.

Read More »

STAA JUSTIN BIEBER AMEREJEA UPYA KWENYE INSTAGRAM



Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Justin Bieber amerudi upya na jina lake lilelile la @justinbieber.

Ila Good Newz inaonekana ujio huu wa kurudi kwenye kurasa yake ya Instagram inaonyesha kwamba Bieber amepewa donge nono kutoka mtandao wa T Mobile ambao ameshindwa kuzuia unono huo.


Read More »

YOUNG KILLER AKIRI JAMBO HILI KUMUHUSU DOGO JANJA

Rapa Young Killer amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli alikuwa ‘Inspired’ kuingia kwenye muziki na msanii Dogo Janja kwani yeye alikuwa anaamini ili msanii aweze kufanikiwa na kutoba kwenye muziki ni lazima awe na umri fulani.

Young Killer alisema hayo jana baada ya kukutanishwa live yeye pamoja na Dogo Janja kwenye kipindi cha FNL ndipo alipokiri kuwa baada ya kuona Dogo Janja ametoboa na kuwa mkubwa ndiyo yeye akaongeza nguvu za mitikasi mpka na yeye akatoka kimuziki.
Dogo-Janja-681x851 (1)-horz
Dogo Janja & Young KIller
“Mimi napendaga kusema ukweli kipindi nahangaika na mishe zangu nilikuwa naamini ili utoboe kwenye muziki ni lazima uwe na umri fulani, sawa Young D alikuwepo na alipata nafasi tukawa tunamuona kwenye matangazo ya show na nini lakini nilikuwa sijaamini kama katoboa.
“Au anaweza kufanya kama tunavyofanya sasa lakini Janjaro alipokuja kutoka ndiyo nikaamini kabisa kumbe unaweza kutoboa ukiwa na hali yoyote muda huo huo na mimi nikaanza kujipanga nikapata mashavu kwa hiyo alikuwa Inspiration kwangu” alisema Young Killer.

Read More »

ONA PICHA ZA VIJIJI 15 VYENYE MVUTO ZAIDI DUNIANI


Tumezoea kuona miji mikubwa ikiwa na muonekano mzuri na ya kuvutia, lakini unaambiwa kuna vijiji pia duniani ni vizuri kwa muonekano,  leo nimekutana na hii list ya vijiji 15 ambavyo vinavutia zaidi duniani.
15. Alberobello- Italy
14. Pariangan-Indonesia
13. Savoca-Italy
12. Göreme-Uturuki
11. Madison-Marekani
10. Júzcar-Spain
9. Reine-Norway

8. Sidi Bou Said-Tunisia

7. Wengen-Switzerland
6. Shirakawa-go-Japan
5. Burano-Italy
4. Bibury-Uingereza
3. Hallstatt-Austria
2. Oia-Ugiriki

1. Eze-Ufaransa


Read More »

RAPA COUNTRY BOY AJA NA BIASHARA HII IFAHAMU HAPA

Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.
Hitmaker wa ngoma ya “Hakuna Matata” Country Boy ameamua kutazama upande wa pili wa biashara tofauti na muziki ikiwa ni katika suala zima la kujitafutia kipato
16229408_313969388998823_4438854391247667200_n
Country Boy
Ikiwa muziki ni biashara ambayo inakwenda na wakati, mkali huyo ameamua kuitazama kwa jicho hilo ili kujiwekea misingi mizuri katika kujipatia kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Yawezekana ndoto za baadhi ya wasanii wengi ni kumiliki migahawa ya Chakula lakini huenda kinachosumbua ikawa ni mitaji au namna ya kuanza biashara hiyo rasmi.
Country Boy ameingia kwenye list ya Wasanii wa Bongo walioamua kuwekeza muda wao katika kutoa huduma ya Chakula na huduma hiyo ameipa jina la Country fast food delivery ambayo kazi yake ni kusambaza chakula kwa yoyote anaehitaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Country Boy alipost ujumbe huu..
Country Boy

Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Inshaallah kesho Tunaanza Country Fast Food Delivery Msosi Heavy Kwaajili Yako Chenye Upishi Mzuri Na Smart Mapishi Ya Kinyumbani Kabisaa”.

Read More »